Knowless aibuka na ushindi wa Primus Guma Guma Super Star S 5

1

Baada ya takriban miezi 6, wasanii 10 waliokuwa wamechaguliwa na waandishi wa habari za burudani, wanafanya nchini Rwanda wanahusishwa katika shindano kali linalowakutanisha wasanii wa hali ya juu (stars), halafu mashabiki wao huchagua msanii bora kuliko wengine, huku majaji wakitoa asilimia 80 kwa kila msanii.

Jumapili hii tariki 15 Agosti 2015 mjini Kigali , Msanii Knowless aliibuka na ushindi wa Primus Guma Guma linaloandaliwa na kampuni ya kutengeneza vinywaji laini na bia Blarirwa.

WA KWANZA KNOWLESS NA WA PILI BRUCE MELODDY

Katika historia ya Shindano hilo, lilianza mwaka 2011 msanii Tom Close ndiye wa kwanza aliyelitwaa, mwaka 2012 likanyakuliwa na King James, mwaka 2013 lilikuwa la Jay Polly, na mwaka jana 2014 Riderman aliibuka na ushindi , mwaka huu wa 2015 limenyakuliwa na Knowless.

MAJAJI

Knowless amezawadiwa kombe na kitita cha milioni 24 Franga za Rwanda, milioni 9 ni pesa tasilimu anakwenda nazo nyumbani halafu zinazobaki zitatumiwa kwenye miradi yake.

DREAM BOYS WALINYAKUA NAFASI YA TATU

Nafasi ya pili ilinyakuliwa na Bruce Melody, alipokea milioni 7,5 Frs na nafasi ya 3 ilinyakuliwa na kundi la Dream Boys lilipokea milioni 7 Frs.
Picha za baadhi ya wasanii.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments