Kigali:Wanahofia kuambukizwa maradhi na malaya kutoka Burundi

3

Wakazi wa jiji la Kigali wanasema kwamba wanahahofia umalaya unaozidi kuongezeka unaofanywa hasa na wasichana wakimbizi kutoka Burundi, na kusema kwamba ni lazima ukomeshwe haraka ili maambukizi ya maradhi yakiwemo ukimwi yasitokee.

Wakazi hawa wanalalamika baada ya miezi michache tangu Rwanda ipokee idadi kubwa ya warundi wanaokimbia nchi yao kutokana na hali ya usalama mdogo na ghasia za kisiasa zinazoendelea nchini Burundi.

Wakazi wa Kigali wanasema kwamba ukahaba ulikuwepo mjini humu, lakini kwamba uliongezeka zaidi wakati warundi walipoanza kukimbilia Rwanda.

Wananchi hao wanasema kwamba wanahofia warundi hao, mienendo yao haijulikani “Tulikuwa tukiona idadi ya wasichana wanaosimamisha wanaume ikiongezeka lakini hatutambui inatokana na nini. Lakini tulifichua kwamba baadhi yao wanaongea lugha ya Kirundi.” Alisema mmoja wa wakazi.

“Kinachoonekana ni kwamba wanatakiwa na wanaume wengi. Serikali ichunguze kwa haraka, wasije wakaleta maradhi yanayoambukiza.” Aliongeza mkazi huyo.

Wakazi wa Kigali kinachowakera ni uwingi wa wanaume wanaotaka kufanya mapenzi na Malaya hao kutoka Burundi. “Ikiwa ni warembo kuliko wanyarwanda, ikiwa wanaomba bei nafuu hatujaelewa.” Mwingine alisema.

Wengi wa Malaya hao kutoka Burundi huwa hawana kazi rasmi, mara nyingi wanapata riziki kutokana na umalaya tu kama wakazi walivyotuambia.

Hata hivyo, Wizara ya wakimbizi na kukabiliana na majanga wiki zilizopita ilitangaza kuwa ni kosa kufanya mapenzi na mkimbizi, kwa kumuonea kutokana na matatizo yake. Na wizara hiyo iliongeza kwamba mkimbizi atakayepatikana akifanya umalaya nchini Rwanda, ataadhibiwa kwa mujibu wa sheria kwani hairuhusuwi.

Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments 3

  1. SubahanaLLAH basi hao malaya watatumaliza, bora serikali ichukuwe hatuwa, bila hivyo ni bala , kwani midada hiyi kama ikiisha jiita mikimbizi huwa haijali itatembeya na midume mingapi ???? balaaaaaaaa

  2. SubahanaLLAH basi hao malaya watatumaliza, bora serikali ichukuwe hatuwa, bila hivyo ni bala , kwani midada hiyi kama ikiisha jiita mikimbizi huwa haijali itatembeya na midume mingapi ???? balaaaaaaaa

Tumia Comments