Utawala bora, usatwi wa jamii na uchumi ndio misingi ya manifesto ya RPF-Inkotanyi

Katibu mkuu wa RPF-Inkotanyi Francois Ngarambe (kati), Msemaji wa Kampeni za uchaguzi Wellars Gasamagera (kushoto) na Kamishna wa RPF Bi Marie Claire Mukasine katika mkutano wandishi wa habari.

Chama kilichopo madarakani nchini Rwanda RPF-Inkotanyi kimetangazia vyombo vya habari misingi ya manifesto yawo katika kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Agosti, mwaka huu.

Jana katika mkutano na wanahabari jijini Kigali, Katibu mkuu wa RPF-Inkotanyi, Mzee Francos Ngarambe, amesema kwamba manifesto yao inalenga kuimarisha uchumi, ustawi wa jamii na uongozi bora kama misingi muhimu ya utawala wao katika miaka saba ijayo.

Ngarambe pia ameahidi wanahabari kwamba mgombea wao atawafikia wananchi nchini kote wakati wa kampeni za uchaguzi zitakazotimua vumbi tarehe 14, Julai yaani keshi ijumaa.

Awali, Tume huru ya uchaguzi ilitangaza rasmi kuwa Rais aliyepo madaraki, Paul Kagame wa RPF-Inkotanyi, Dk Frank Habineza na Philipe Mpayimana(Mgombea huru) ndio watu waliotimiza vigezo na masharti ya kuwania kiti cha urais .

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments