Polisi yaanza kusaka mtu aliyesema kwenye Facebook kuwa Dr Frank Habineza anastahili kuwa Rais wa sokwe.

Waziri wa sheria Nchini Rwanda Bw Jonhston Busingye

Waziri wa sheria Bw Jonhston Busingye ameviambia vyombo vya habari kwamba Polisi nchini Rwanda imeanza kusaka mtu aliyesema kwenye Facebook kwamba Dk Frank Habineza, mgombea urais wa chama cha kuhifadhi mazingira (Green Party),kwamba yeye hafai kuwa Rais wa wanyarwanda ila sokwe wa milimani.

Wiki iliyopita, Habineza aliagiza serikali kuchukua hatua dhidi ya mtu anayejitambulish kama Chantal kwenye Facebook kwa kuwa alimtumia ujumbe wa kibaguzi.

Mtu huo aliandika ‘’kwa upande wangu, wewe unastahili kuongoza sokwe wetu wa milimani kwani nawo wanahitaji kiongozi’’

Akiongoea na wana habari jana kwenye makao makuu ya Polisi, Waziri Busingye alisema kwamba Polisi imeanza kusaka mtu huwo ili adhibiwe na liwe funzo kwa watu wote wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii.

‘’Tuliitaka Polisi kutafuta mtu huo na ijuwe mahali ujumbe huo ulipotoka, Nadhani mtu huo anaishi nje ya Rwanda . Lakini iwapo anaishi nje tuataendelea kumsaka kwa ushirikiano na watu mbalimbali.’’ alisema Johnston Busingye.

Sheria husema kwamba mtu anayetenda dhambi la kutukana hadharani, hufungwa miezi sita gerezani na kutoa adhabu ya Frw 500.000 hadhi Rwf 3.000.000.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments