Bara la Afrika latakiwa kuwa na sauti moja - Rais Kagame

Rais Kagame amesema kwamba masuala yaliyomo katika kila nchi barani Afrika hatayakiwi kuwa kikwazo cha kutokuwa pamoja na kujiendeleza.

Haya ameyatangaza jumatano wiki hii katika baraza la bunge la Djibouti akikamilisha ziara ya siku 2 katika nchi hiyo.

Rais Kagame amebaini kuwa mataifa yanaweza kuwa na sauti moja katika kutatua matatizo yanayozikumba nchi hizo.

Ameongeza kuwa mataifa yaliyopiga hatua ni mataifa yaliyotambua matatizo yao kuyatafutia ufumbuzi, kusikiliza wananchi na historia.

Rais Kagame alirejelea ujumbe aliotoa kwa wakuu wa mataifa katika jumuiya ya umoja wa Afrika AU, akisema kwamba mabadiliko katika mataifa ya bara hili yanatakiwa ili jumuiya ya Umoja wa Afrika idumu na iwe na uwezo.

Amefurahia uhusiano wa Rwanda na Djibouti, amesema cha msingi na lengo la mataifa haya ni ushirikiano na mawasiliano kwa wananchi wa pande mbili.

Amewaelezea wabunge kwamba bara la Afrika lina kila kitu cha kujivunia kwa maendeleo ya nchi.

Kabla ya kukamilisha ziara yake, rais Kagame alitembelea bandari ya Doraleh iliyopo km 5 magharibi mwa mji mkuu wa Djibouti.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments