BASKETBALL : Rwanda yapewa tikiti ya kushiriki kombe la Afrika 2017

By Christopher Karenzi

Timu ya taifa ya Rwanda ya mchezo wa kikapu tayari imekata tikiti ya kushiriki mashindano ya kombe la mataifa barani Afrika 2017 yatakayofanyika Congo Brazza-Ville mwezi Augosti 2017.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika mkutano mjini Abidjan nchini Cote d’Ivoire jumanne wiki hii na kuidhinisha mataifa yatakayoshiriki mashindano hayo.

Katika mkutano huo, Rwanda na Guinea ni mataifa mawili yaliyopewa kadi inayofahamika kama (Wild Card) ya kushiriki baada ya kudhihirka kwamba timu hizo zilifanya vema katika kanda (Zones), Rwanda ilikuwa imeondolewa katika ukanda wa 5 (Zone 5) ambapo ilimaliza kwenye nafasi ta tatu.

Timu hizo 2 zinafuata zingine 14 zilizokuwa zimefuzu kushiriki kombe la mataifa
2017 (FIBA AfroBasket 2017). Shindano hilo litafanyika nchini Congo Brazza Ville kuanzia tarehe 19-30 Augost 2017.

Droo ya michuano hiyo itafanyika mwezi huu wa Aprili 2017 kwa mujibu wa tovoti ya FIBA-Afrique.

Rwanda na Guinea zinafuata wenzao wa Nigeria mabingwa msimu uliopita, Angola, Cameroon, Cote d’Ivoire, jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Misri, Mali, Morocco, Msumbiji, Senegal, Tunisia, Uganda, Congo Brazza Ville na Afrika ya Kusini.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments