Half marathon : Nyirarukundo anyakua medali ya dhahabu

Salome Nyirarukundo

Mwanariadha chipukizi wa kike Salome Nyirarukundo ameshinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Berkane International Half Marathon yanayofanyika nchini Morocco kwa mara ya tatu.

Salome,19, ameshinda hii meadli ya dhahabu akitumia saa moja dakika 11 na sekunde 13 kwa kukimbia umbali wa kilomita 21.097 akitumia na kuvunja rekodi iliyowekwa na Mwethipia Olira Belyenesh aliyetumia saa moja, dakika 11 na sekunde 18.

Nyirarukundo ameshika nafasi ya kwanza juu ya Mwethipia na Mkenya akitumia saa mija dakika 11 na sekunde 13.

Mwaka jana, Nyurarukundo alishinda medali ya shaba kwenye mbio za Silvesterlauf aliyofanyika nchini Ujerumani.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments