Wanao itikadi ya mauji ya kimbari, wao hawana nguvu. – Mbunge Karenzi

Mkuu wa tume ya kupambana na mauji ya kimbari katika bunge la Rwanda, Mbunge Theoneste Karenzi amesema kwamba idadi ya watu wanao itikadi ya mauji ya kimbari ilipungua mno na wao hawna nguvu hata kama jitihada za kupambana nao zinapswa kuongezwa.

Katika mkutano wa hao wabunge uliofanyika Ijumaa iliyopita katika jingo la Bunge, Bw Karenzi alisema kwamba watu wanao itikadi ya mauaji ya kimbari wanaishi barani Ulaya kwa uingi kuliko ndani mwa Rwanda.

Na aliongeza kwamba ni lazima jitihada zitumike kwa kutafuta washiriki nje ya nchi watakaosaidia kupambana na hao watu wanaobaki na itikadi mbaya ya kukana mauji ya kimbari dhidi ya watutsi iliyotokea mnamo mwaka 1994 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya milioni moja.

Rwanda inakaribia kukumbuka mauaji ya kimbari kwa mara ya 23, mwezi Aprili,7

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments