Mbanda aliyesubiriwa kuwasili Rwanda, hajafika.

Jean Daniel Mbanda aliyetangaza kuwasili nchini Rwanda kwa ajili ya Uchaguzi urais Jumatano usiku, yeye bado hajatua uwanjani wa ndege wa Kigali.

Mbanda,65, anayeishi uhamishoni nchini Kanada alitangaza nia yake ya kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti, 4,2017.

Akitumia ukurasa wake wa Facebook, Mbanda amesema kwamba ameshindwa kuchukua ndege kuja Rwanda kwa sababu zake binafsi zisipo za kukatazwa na serikali ya Rwanda, kitu Nahimana alichoita sababu ya kushindwa kurejea nchini Rwanda.

Jean Mbanda ni mtu wa nne baada ya Thomas Nahimana, Frank Habineza na Philipe Mpayimana waliotangaza nia yao ya kushiriki uchaguzi urais wakitoka katika upinzani.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments