Ndege ya RwandAir kuruka hadi Uingereza.

Shirika la ndege nchini Rwanda, RwandAir, limetangaza kuwa ndege yao aina ya Airbus A330 itaanza kupaa anga kwelekea Uingereza ambapo itatua kwenye uwanja wa ndege wa Gatwick International Airport jijini London, mwezi Mei.

Taarifa iliyotolewa na RwandAir inaeleza kwamba hii itakuwa njia ya moja kwa moja kwenda London pasipo kupita nchini nyingine.

‘’ Tuna furaha nyingi kwa kuweza kufanikiwa na kufungua njia ya mara kwa mara kwenda London, hii ni kwa nia kabambe ya kuhudumia vyema wateja wetu’’ John Mirenge, mkuu wa RwandAir amesema.

Awali, RwandAIR imeshatangaza kwamba ndege zao zitaanza kuruka kwenda Mumbai, Uhindi na Harare, Zimbabwe katika wiki mosi ya Aprili,2017

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments