Kagame ahutubia mkutano wa AIPAC Policy Conference

Jana, Jumapili tarehe 27, mwezi Machi, 2017 Rais Paul Kagame amehutubia mkutano wa AIPAC Policy Conference uliofanyika nchini Marekani.

Katika mkutano huo ambao ulivutia washiriki zaidi ya 18,000 Rais Paul Kagame alitoa wito mshikamano kimataifa dhidi ya ukanaji wa mauji ya kimbari na kunyanyasa manusura ili dunia iendelee kuwa salama.

‘’usalama wa watu waliowahi kulengwa na ukatili hauwezi kuwa kimwili pekee ila na kiakili. Ushindi wa itikadi kali ni kushindwa kwa uzalendo.’’ Yeye amebaini.

‘’tukiwa pamoja na marafiki kama Marekani, tunapaswa kupaaza sauti kwa mshikamano kimataifa dhidi ya jitihada zinzotumiwa kwa kukana mauji ya kimbari na kuwanyanyasa manusura.’’ Aliongeza.

Rais Kagame amesema kwamba anaiunga mkono nchi ya Israel ambayo inakabiliwa na vitisho kutoka kwa baadhi ya majirani akisema kwamba nchi ina haki ya kuishi na kustawi kama mwanachama kamili wa jumuiya ya kimataifa.

Baada ya kuhutubia mkutano wa AIPAC, Rais Paul Kagame amevunja rikodi ya kuwa ndiye Rais pekee kutoka bara la Africa aliyetoa hotuba katika mkutano huo.

Mkutano mkuu ujulikanao kama AIPAC Policy Conference huandaliwa na Israel kwa ajili ya kutafakari uhusino wake na Marekania

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments