Rais Kagame akutana na Mkuu wa Benki ya Dunia.

Rais Paul Kagame apokea Dkt Kim Yong Jim anayeongoza Benki ya dunia katika ikulu ya Rwanda wakati alipohitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Rwanda.

Baada ya mazungumzo ya faragha na Rais Paul Kagame, Bw Kim aliahidi kwamba Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana kwa karibu na Rwanda kwa kuwa Rwanda ni nchi inayo sera kabambe za uchumi na ni nchi inayo mwelekeyo mzuri kuliko mataifa mengine.

‘’licha ya kutokuwa na maliasili ya kutosha, Rwanda ilifanikiwa kupiga hatua kiuchumi kuliko mataifa mengine duniani, kwa hivyo mimi sina shaka ya kuwa uchumi wa Rwanda utaendelea kukua nasi tutaendelea kushirikiano karibu na Rwanda katika mipango mbalimbali ya uchumi .’’ Yeye alisema.

Waziri wa mipango na fedha, Balozi Claver Gatete alisema kwamba ujio nchini Rwanda wa Bw Kim ni ishara ya kuonyesha ushirikiano mzuri ulioko kati ya Rwanda na Benki ya Dunia.

Akiwa nchini Rwanda, Dkt Kim Yong Jim alizuru mradi wa ndege zisizo rubani wilayani Muhanga ambazo hutumiwa kwa kusambaza damu katika maeneo ya milimani, eneo la viwanda na kadhalika.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments