Rwanda kuongeza idadi ya walinda amani Sudan Kusini

Luteni Kanali Rene Ngendahimana
Msemaji wa jeshi la Rwanda, Luteni Kanali Rene Ngendahimana amethibitishA kuwa Rwanda iko tayari kutuma kikosi cha walinda amani nchini Sudan Kusini.

Ngendahimana alisema hayo jana baada ya kukutana jijini Juba,Jumanne na Herve Ladsous, Kamanda wa vikosi vya wa walinda amani vilivyopo Sudani Kusini chini ya UNAMISS.

Yeye alisema kwamba vikosi vya walinda amani kutoka Rwanda, Nepal, na Banglagesh vataanza kumiminika nchini humo wiki chache zijazo.

Mwaka jana, Baraza la usalama duniani liliomba mataifa yanayolinda amani nchini humo kuchangia Askari wengine 4,000 kwa ajili ya kushughulikia mzozo wa kisiasa unaodumu mda mrefu katika nchi hiyo changa duniani.

Licha ya UN kuamuru askari 4,000 wa nyongezo, uliomba Rais Kiir kutumia njia za kisiasa kwa kutatua vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini mwake kuliko nguvu za kijeshi.

Na mpaka sasa Rwanda inayo walinda amani 1,650 nchini Sudani kusini.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments