Rais Paul Kagame ajivunia hatua iliyopigwa na Papa Francis

Rais Paul Kagame akiwa na Jeannette Kagame walikutana na Papa Francis katika Vatican
Jana Rais Paul Kagame ametembelea makao makuu ya kanisa Katoliki mjini Roma ambapo alikutana na Papa Francis.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba msamaha kwa Kanisa kushindwa kuzuia mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994 lakini pia kwa viongozi wa Kanisa hilo ambao huenda walihusika.

Akitumia ukurasa wake wa twitter, Rais Paul Kagame amesema kwamba kuomba radhi kwa makosa ni kitendo cha ujasiri na maadili.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments