Papa aomba msamaha kwa niaba ya kanisa Katoliki nchini Rwanda

Rais wa Rwanda Paul Kagame akikutana na Papa Francis, Jumatatu hii, Machi 20, 2017, mjini Vatican.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba msamaha kwa Kanisa kushindwa kuzuia mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994 lakini pia kwa viongozi wa Kanisa hilo ambao huenda walihusika.

Papa Francis ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na rais Paul Kagame katika makao makuu ya Kanisa hilo mjini Vatican.

Kiongozi huyo amesema kuwa amemwomba Mungu kuwasamehe viongozi wa Kanisa hilo na watu kutoka jamii ya Wakiristo wengine walioshindwa kuwajibika na kuzuia mauaji hayo ya zaidi ya watu milioni moja wa kabila la Kitutsi.

Serikali ya Rwanda mwezi uliopita, iliitaka Kanisa Katoliki kuomba radhi kutokana na kuhusika kwao katika mauji hayo mabaya katika historia ya Rwanda.

Mwezi Novemba mwaka jana, Kanisa Katoliki liliomba radhi kwa kuhusika katika mauaji hayo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments