Rwanda Democratic Green Party kuiga sera za Trump iwapo wakashinda urais

Tangu kushoto, Dkt Frank Habineza, raisi wa chama cha demokrasia na kuhifadhi mazingira na Jean Claude Ntezimana, mkuu wa mawasiliano

Chama cha Demokrasia na kuhifadhi mazingira nchini Rwanda kimetangaza kujenga uzio kwa ajili ya kulinda usalama wa Rwanda iwapo wakashinda urais mwaka huu.

Katika mkutano mkuu wa wakerektwa wa Green Party uliofanyika tarehe 19, Machi,2017, Jean Deo Tuyishime ambaye ni msimazi wa mawasiliano, amesema kwamba iwapo chama chake kushinda urais, wao watajenga ukuta utaotenganisha Rwanda na mataifa jirani kwa kuzuia makundi yenye silaha kuvamia ardhi ya Rwanda.

Hii sera ya kujenga uzio kwa ajili ya usalama wan chi ni sawa na ile ya Donald Trump, Rais wa Marekani, ambayo ilikosolewa pakubwa na wadau wa kisiasa wakisema haina maana.

Na katika mkutano huo, Dkt Frank Habineza amaidhinishwa rasmi kuwa ndiye mgombea atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi urais unaotarajiwa kufanyika mnamo mwezi Agosti, 4.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments