Rais Paul Kagame ziarani Vatican

Rais Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame amewasili Jumapili hii jioni katika mji wa Roma kwa ajili ya mkutano wa Jumatatu na Papa Francis. Ofisi ya rais wa Rwanda ndio imetangaza ziara hiyo kwenye akaunti yake ya Twitter.

Mkutano huo ulikuwa kwenye ajenda rasmi ya kiongozi wa Kanisa Katoliki, Jumapili jioni. Kwa mujibu wa Ofisi ya rais wa Rwanda, Paul Kagame atafanya ziara katika mji wa Roma kwa mwaliko wa Papa Francis kwa majadiliano juu ya "mahusiano baina ya Rwanda na Vatican."

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments