Maharamia waiachia huru meli pwani ya Somalia

Maharamia waiachia huru Meli

Maharamia wa Kisomali wameiachia huru meli ya mafuta waliyokuwa wameikamata kwenye pemba ya Afrika siku ya Jumatatu bila ya kulipwa fedha.

Maafisa nchini Somalia wamesema wafanyakazi saba wa meli hiyo raia wa Sri Lanka waliachiwa pia bila ya kudhuriwa.

Meli hiyo ilikamatwa katika eneo la pwani ya Puntland siku ya Jumatatu, ikiwa ni mara ya kwanza katika eneo hilo katika kipindi cha miaka mitano.

Maharamia hao waliiachia meli hiyo baada ya mazungumzo yao na askari wanamaji wa Puntland.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments