Rwanda kuenyeji mafunzo ya kijeshi barani Africa

Wanajeshi kutoka mataifa mbalimbali barani Africa wanatarajia kumiminika nchini Rwanda kwa kuhudhuria mafunzo ya kijeshi yatakayoanza mwezi huu, tarehe 20 nchini Rwanda.

Haya mafunzo yanalenga kujengea uwezo kimafunzo wa kutoa msaada wa dharura wakati wa mgogoro barani vikosi vya ACRC (Africa Capacity for Immediate Response).

Mkutano wa maandalizi umefunguliwa mjini Kigali jumatatu iliyopita na Meja Jenerali Martin Nzaramba, mkuu wa majeshi ya Rwanda ngome ya Nasho, kwa niaba ya Rwanda.

Jenerali Nzaramba ambaye atakuwa mkuu wa mafunzo, amesema kwamba mafunzo yatakuwa fursa muhimu kwa viongozi wa Africa ya kuonesha nia ya pamoja ya kujitafutia suluhu sisi wenyewe kama waafrica.

Nzaramba amesema kuwa ‘’utulivu Africa III’’ ni ishara mwafaka kwa nchi wanachama wa ACRC ya kujijengea uwezo wa kijeshi kwa ajili ya kutimiza ndoto za kutafutia ufumbuzi matatizo yanayosumbua bara la Africa.

Akinukuu Rais Paul Kagame, Kanali Arry Katimbe aliyesema kwa niaba ya umoja wa Africa. alisema kwamba Waafrica ndo pekee wanatarajia kutatua matatizo yanayowakumba.

Mpaka sasa, mataifa yenye hiari ya kushiriki mafunzo haya ni Algeria, Angola, Benin, Burkina Faso, Chad, Misri, Niger, Rwanda, Senegal, Afrika kusini, Sudan, Tanzania na Uganda.

Kanali Nzaramba Martin

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments