Rais Kagame kupewa tuzo ya ushirikiano bora na wayahudi

Rais Paul Kagame akiwa pamoja na (kuanzia kushoto) Rabbi Shmuley Boteach, Elie Wiesel
Rais Paul Kagame anatarajia kuvishwa medali ambayo hutajwa jina la Dr. Mariam na Sheldon G. kwa kuwa ndiye rais duniani aliyefanikiwa na kushirikiana vyema na Wayahudi.

Paul Kagame atapewa tuzo hii na shirika la The World Values Network (linalotetea haki za wayahudi) lililoanzishwa na Rabbi Shmuley Boteach katika sherehe zitakazofanyika mjini Manhattan, nchini Marekani mnamo mwezi Mei, 21, 2017.

Shmuley anasema kwamba Rais Paul Kagame atapewa medali hii kwa ajili ya kumshukuru jinsi alivyopambana na mauaji ya kimbari na kuwa ni mmoja wa viongozi duniani kote aliyeshirikiana vyema na nchi ya Israel.

Rais Paul Kagame anasifiwa kuwa ndiye rais aliyekubari kuweka maisha yake hatarini kwa kusimamisha mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi katika mwaka wa 1994.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments