AERG na GAERG mbioni kujindaa kuadhimisha mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi kwa mara ya 23

Jukwaa la vijana wanusurika wa mauji ya kimbari : wanavyuo, wanafunzi wa mashule ya sekondari na waliokuwa wanajukwaa wako katika maandalizi ya kuadhimisha mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yaliyotokea mnamo mwaka 1994 ambapo watu zaidi ya milioni waliuawa kinyama.

Katika "AERG GAERG Week" inayotarajiwa kuanza jumamosi, mwezi huu, wao watafanya hatua mbalimbali zikiwemo kuwajengea nyumba wajane wanusurika,… kwa ajili ya kuwatia moyo katika hii hali ngumu tunayokaribia.

Olivier Mazimpaka, rais wa GAERG, amesema kwamba wiki hii itakuwa wakati muhimu wa kuunga mkono pendekezo la nchi la kujiendeleza.

‘’EARG-GAERG week’’ itafanyika katika majimbo yote ya nchi. Katika jimbo la kusini ni katika wilaya ya Ruhango, maghribi ni katika wilaya ya Nyaruguru, mashariki ni katika wilaya ya Nyagatare, kasikazini itafanyika katika Rubavu na jijini Kigali wao watakuwa katika Kicukiro.

Tangu AERG-GAERG week kuanza katika mwaka wa 2015, nyumba 17 zilijengwa na nyingine 65 zilikarabatiwa, ng’ombe 21 zilipewa manusura na barabara yenye umbari wa kilomita 13 ulijengwa.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments