Meya mstaafu wa wilaya ya Gicumbi atiwa mbaroni

Alexandre Mvuyekure aliyekuwa meya wa wilaya ya Gicumbi, iliyoko kasikazini mwa Rwanda atiwa nguvuni kwa ombi la mashtaka kama ACP Theos Badege ambaye ni msemaji wa jeshi la polisi la Rwanda alivyotangazia Makuruki.rw.

Habari ambayo haijathibitishwa inasema kwamba Mvuyekure anakabiliwa na makosa kimatumizi ya fedha za serikali katika shughuli zake binafsi.

Msemaji wa upande wa mashataka, Faustin Nkusi ameiambia Makuruki.rw kwamba yeye hajakusanya habari kamili kuhusu kukamatwa kwa kiongozi huo lakini naye amethibitisha kwamba Alexandre ametiwa nguvuni na polisi ya Rwanda.

Hii si mara ya kwanza yeye kukamatwa kwani mwaka jana mnamo mwezi Julai alikamatwa akishtakiwa ubadhirifu wa fedha za VUP na kutumia nyaraka bandia.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments