Rais Paul Kagame awatembelea wanyarwanda wanaoishi nchini Uingereza.

Hapo jana jumanne, Rais Paul Kagame aliwatembelea wanyarwanda wanaoishi nchini Uingereza wakati alipokuwa njiani akielekea Marekani kwa kuitikia mwaliko wa chuo cha havard ambapo yeye anatarajia kuzungumza na wanachuo kuhusu maswala mbalimabli.

Katika ufalme wa Malikia Elizabeth wa pili, Bw Paul Kagame alipokewa kwa shangwe na mbwembwe na wanyarwanda waliosimama kando kando ya barabara alipopitia na yeye aliwaambia kuwa alipita Uingereza kwa kuwapungia mkono tu na kuwashukuru jinsi wanavyo peperusha vyema bendera ya nchi.

Rais Paul Kagame aliwaahidi kwamba yeye atarudi tena kwa ajili yao tu na wengi wao walipiga juu sauti wakisema kwamba wanataka tukio la ‘’Rwanda day’’ lifanyike nchini humo wakati ujao.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments