Bw. Kavaruganda ndiye balozi wa Rwanda nchini New Zealand

Balozi wa Rwanda anaye makao makuu nchini Singapore, alitoa barua ya kujitambulisha kwa Dame Patsy Reddy, Gavana mkuu wa New Zealand kwamba ndiye balozi wa Rwanda nchini New Zealand , jumatano iliyopita.

Hii Sherehe ilifanyika katika jengo la serikali lililopo jijini Wellington, huu ulikuwa wakati wa kutafakari uhusiano uliyopo kati ya mataifa mawili na kushukuru nchi ya New Zealand kwa kuwa ilikuwa kwenye mstari wa mbele kwa kusaidia Rwanda kujiunga na commonwealth na kuwa mwanachama asiye kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Katika mkutano wa faragha, Balozi Kavaruganda na Bi. Dame walijadili jinsi ya kuimarisha uhusiano kiuchumi, kilimo, nishati, utalii na kukuza uwekezaji baina yamataifa mawili.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments