Mbivu na mbishi kati ya Rayon Sports na APR FC kujulikana leo

Leo ni sikukuu ya mashujaa nchini Rwanda lakini leo hakutakuwa sherehe kwa mahasimu wa jadi.

Rayon Sports na APRFC watashuka dimbani tena baada ya siku chahce tu APR FC kuichapa Rayon Sports bao moja kwa nunge katika mchezo wa ligi kuu.

Na wao walikuwa wakichuana kwa alama lakini leo ni pesa ambapo mshindi atapewa Rwf 3 milioni na mshindwi atapewa Rwf 1.5 milioni.

Huu utakuwa mchezo wa tatu kati ya hawa vigogo wa kabumbu nchini Rwanda na APR FC ilishinda michezo miwili mfululizo sasa, leo itamalizikaje ?

Hata hivyo, Rayon Sports inaongoza jedwali ya ligi kuu na alama 36, APR FC ni ya pili na alama 34.
na mfungaji bora ni Nsengimana Danny ambaye ni mchezaji wa Police Fc.

Wafungaji bora

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments