Mgombea wa upinzani ametua Rwanda kwa kuwanaia urais

Mpayimana Philipe aliyetangaza kushiriki katika uchaguzi urais utakaofanyika mwezi Agosti, mwaka huu amefika nchini Rwanda katika usiku wa manane.

Mpayimana anaeishi nchini Ufaransa amefika katika uwanja wa ndege wa Kanombe saa saba na unusu za usiku aliko pokewa na mashabiki wake.

Yeye ameambia wana habari kwamba yeye yuko tayari kupambana vikali na Rais Paul Kagame anayekalia kiti cha urais miaka 16 iliyopita.

Mwaandishi wa vitabu, pia mtangazaji wa zamani kwenye redio alionesha hisia zake za kushiriki uchaguzi mkuu mwaka jana mwezi Oktoba, 31.

Na ni mgombea urais wa pili kutoka upinzani aliyeelezea nia yake ya kushiriki uchaguzi urais baada ya Dkt Frank Habineza wa chama cha mazingira na demokrasia, Rwanda Democratic Green Party.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments