Dkt. Harebamungu kuwakilisha Rwanda nchini Mauritania

Dkt. Mathias Harebamungu alijitambulisha kwa Rais wa Mauritania Mhe. Mohamed Ould Abdel Aziz kama balozi wa Rwanda nchini humo.

Dkt Mathias alitoa barua ya kujitambulisha katika sherehe iliyofanyika tarehe 23, mwezi Janauri, 2017 katika ikulu ya Mauritania.

Balozi alishukuru jinsi alivyopekwa na aliahidi kufanya lolote liwezekanalo kwa kuimarisha urafiki baina ya Rwanda na Mauritania.

Wakati huo huo, Rais Abdel Aziz alipokea mabarua ya mabalozi wa Yemen, Pakistan, Sri-Lanka, Danmark, Hongary, Romania na Finland.

Kama kawa, Dkt Mathias atabaki kuwa balozi wa Rwanda katika Senegal na Mali.

Dkt Mathias Harebamungu akitoa barua kwa Rais Mohamed Ould Abdel Aziz.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments