Ivan Minnaert asaini mkataba katika Mukura VS

Mbelgiji Ivan Minnaert aliyewahi kuifunza Rayon Sports Fc amesaini mkataba wa kuifunza Mukura VS inayoishi wilayani Huye kusini mwa Rwanda.

Kocha huyo amesaini mkataba wa miezi sita baada ya kiwang\o cha Okoko Godefroid kuota nyasi katika Myukura VS kwa kukosa mafanikio.

Minneart ametakiwa kuisadia Mukura kuchukua nafasi ya juu kwenye jedwali la ligi kuu ya Rwanda na kuisaidia kufika mbali katika kombe la amani kama Niyobuhungiro Fidele, afisa wa mawasiliano alivyo ambia Makuruki.rw.

Ivan Menneart aliwahi kufunza Rayon Sports mwezi novemba mwaka wa 2015 kabla ya kuajiliwa na Leopards ya Kenya na akatimuliwa mwezi Novemba mwaka jana.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments