Evode Imena ametiwa nguvuni

Bw Evode Imena aliyekuwa katibu wa serikali katika wizara ya ardhi, misitu na maliasili ametiwa nguvuni pamoja na watu wengine wasiofahamika wakishukiwa na makosa yaliyotokea katika uchimbaji migodi.

Imena Evode aliyekuwa katibu wa serikali katika MINIRENA anayehusika na uchimbaji migodi alitimuliwa mwezi Oktoba mwaka jana baada ya Rais Paul Kagame kufanya mabadiliko makubwa ya serikali ya Rwanda.

Polisi imethibitisha habari hii, Theos Badege ambaye ni msemaji wa polisi ya Rwanda amesema kwamba Bw Imena alishikiliwa ijumaa iliyopita.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments