Wapiganaji 30 wa M23 wakimbilia Rwanda

Mojawapo ya waliokuwa waasi wa M23
Kundi la wapiganaji wanaosema kuwa wapiganaji wa kundi la M23 wamekimbilia nchini Rwanda hii jumapili kupitia mpaka uliopo kati ya Rwanda na DRC magharibi mwa Rwanda kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Rwanda.

Hawa waasi wanasema kwamba wanakimbia mapigano yanayofanyika nchini mwao

Msemaji wa majeshi ya Rwanda, Luteni kanali Rene Ngendahimana amesema kuwa hawa wapiganaji walitambuliwa na shirika la msaraba mwekundu na kuwa wao wana matatizo ya kiafya.

Awali Serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya kongo imeshutumu nchi ya Uganda kusaidia waasi wa M23 kuishambulia wakitumia mpaka uliopo kati ya hayo mataifa mawili lakini uongozi wa Uganda ulitupilia mbali madai hayo.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments