FERWAFA mbioni kumteua kocha mkuu.

Shirikisho la Kandanda nchini Rwanda, FERWAFA ,limetangaza kuwa limeanza pilika pilika za kumteua kocha mkuu wa timu ya taifa .

Masharti ni kwamba anayeweza kuwania ajira hii anatakiwa kuwa na cheti cha digri ya A inayotolewa na shirikisho la kabumbu duniani, FIFA.

Kocha atakayechaguliwa, atajaza pengo lililoachwa na McKinstry aliyetimuliwa mwaka jana kwakushindwa kufuzu timu ya taifa kombe la Afrika linalofanyika nchini Gabon wakati huu.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments