Rwanda yaongoza katika vita dhidi ya ufisadi Afrika Mashariki

Ingabire Immaculee, mkuu wa shirika la Transparency Intewrnational Rwanda

Rwanda inaongoza katika vita dhidi ya ufisadi kati ya mataifa 6 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Transparency International

Tanzania ni ya pili lakini ni ya 116 duniani, Kenya ya tatu lakini ya 145 duniani.
Rais wa Tanzania John Magufuli hivi karibuni, alizindua Mahakama maalum ya kusikiliza kesi za ufisadi, huku Kenya ikazindua mahakama kama hiyo kama hiyo ambayo imeonekana kutofanya kazi vizuri miaka iliyopita.

Uganda inashikilia nafasi ya nne na ya 115 huku Burundi ikiwa ya nne na ya 159 huku Sudan Kusini ikiwa ya mwisho na ya 175 duniani.

Somalia inasalia kuwa taifa fisadi zaidi duniani, ikifuatwa na Sudan Kusini, Korea Kaskazini, Syria na Libya.

Bostwana inaongoza barani Afrika kwa taifa linalopambana vilivyo na ufisadi, ikifuatwa na Cape Verde, Mauritius na Rwanda.

Hata hivyo, mataifa yanayofanya vizuri katika vita dhidi ya ufisadi ni pamoja na Denmark ambayo inaongoza, ikifutawa na New Zealand, Finland, Sweden, Switzerland, Norway, Singapore, Uholanzi Canada na Ujerumani.

Transparency International inasema mataifa mengi yanashindwa kupambana na ufisadi kutokana taasisi zilizopewa jukumu hilo kutowajibika ipasavyo.

Hata hivyo, Bi Ingabire Marie Immaculée, mkuu wa shirika la Transparency International Rwanda, amesema kwamba ingawa si vibaya Rwanda kushika nafasi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki lakini inapaswa kuongeza juhudi za kupambana na ufisadi kwa kuchukua nafasi ya kwanza barani Afrika na hata duniani kote.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments