Unga yamweka P Fla gerezani mwaka mmoja

Rapa P.Fla anayejulikana kuwa mmoja wa wanzilishi wa kundi la Tuff Gangs amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada ya kukutwa hatia na matumizi ya madawa ya kulevya.

Hakizimana Murerwa Amani anayejulikana kwenye jina la P.Fla alikamatwa na polisi mwezi Desemba, 13, 2016 papo kwa papo akitumia bangi na hivi sasa anafungwa gerezani ya 1930 iliyopo mjini Kigali.

Mama yake Nzamukosha Hadidja alithibitisha habari hii kwa vyombo vya habari. Yeye alisema mwezi Januari, 20,2017 ndo mahakama ilimhukumu mwanae kifungo cha mwaka mmoja jela.

P.Fla ni mtoto wa Nzamukosha Hadidja aliyekuwa mtangazaji wa redio Rwanda na redio Huguka na Al Hajj André Habib Bumaya aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Rwanda.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments