California : Balozi Mukantabana ahimiza wanyarwanda kuhudhuria uchaguzi urais

Bi Mathlide Mukantabana amehimiza wanyarwanda kuhudhuria kwa uingi uchaguzi urais utakaofanyika mwezi Agosti, 3, 2017 kwa wanyarwanda wanaoishi katika nchi za ugenini.

Mathlide amesema hayo mjini Davis uliyopo katika jimbo la California nchini Marekani alipo kutana na wanyarwanda wanaoishi humo kwa minajili ya kuwakumbusha jinsi msaada wao ni mchango muhimu kwa kujenga taifa lao la kuzaliwa.

Mathlide aliwashukuru jinsi walivyohudhuria RwandaDay iliyofanyika mjini San Francisco na alipata fursa ya kuwakumbusha kujivunia kuwa Rwanda iliweza kutumia ndege zisizo rubani katika shughuli za afya na mapokezi bora ya mkutano mkuu wa umoja wa Afrika ulio fanyika mjini Kigali mwaka huu.

Balozi huo aliwaambia kwamba miaka mitatu iliopita wanyarwanda walianza mchakato wa kutaka katiba ibadilike ili kuruhusu Rais Paul Kagame kuwania muhula mwingine. Hatimae wao walipiga kura ‘’ndio’’ inayomaanisha kuwa wanyarwanda wanahitaji kuendelea kuongozwa katika amani na utulivu.

Kuhusu mambo ya uchaguzi, Bi Mathlide Mukantabana aliambia washiriki kwamba kupiga kura ni haki kila Mnyarwanda asiyoweza kunyimwa.

Katika mkutano huu, Balozi Mukantabana alikuwa pamoja na Lawrence Manzi ambaye ni mshauri wa kwanza katika ubalozi wa Rwanda nchini Marekani.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments