Warundi 12 waokolewa Polisi ya Rwanda.

Jana kwenye makao makuu, jeshi la polisi la Rwanda limevionyesha vyombo vya habari warundi 12 wakiwemo wanawake 11 na mwanaume mmoja waliokamatwa na polisi ya Rwanda mwezi januari, 10, 21017 kwenye mpaka wa Kanyaru uliopo kati ya Rwanda na Burundi wakisafirishwa kuuzwa(Humana Traffiking) barani Asia kupitia Rwanda.

Polisi imesema kwamba hawa watu 12 walikamatwa wakiwa pamoja na wakenya watatu wanaodaiwa kuhusika na uhalifu wa mauzo ya binadamu.

Akiongea na wanahabari kwenye makao makuu ya polisi, mojawapo ya walio okolewa alisema kwamba yeye aliambiwa kuwa akifika nchini Oman yeye atapewa kazi.

Naibu msemaji wa polisi, Chief Spt Lynder Nkuranga, alisema kuwa waathirika walikamatwa mpakani wakisafirishwa nchini Saudi Arabia, Oman na Qatar.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments