Padri Thomas Nahimana atangaza kuunda serikali uhamishoni

Padri Thomas Nahimana anayedai kukataliwa kurejea nyumbani kwa kuanza mchakato wa kushriki uchaguzi urais unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti, mwaka huu ameiambia sauti ya Amerika kwamba yeye na washirika wake wanajianda kuunda serikali uhamishoni ambayo itawasaidia kueleza haki yao na matatizo yanayowakumba.

Nahimana ambaye ni katibu mkuu wa chama cha kisiasa ‘’Ishema Party’’ alitarajiwa kuchukua ndege nenda Rwanda lakini yeye ameiambia redio hii ya Marekani kuwa amekataliwa kuchukua ndege katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels nchini Ubelgiji kwa ombi la Rwanda.

Hata hivyo, Balozi wa Rwanda nchini Ubelgiji, Mhe Olivier Nduhungirehe ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook kwamba Nahimana anasema uongo kwani yeye hakuwa kunyimwa haki ya kurejea nchini Rwanda na ameongeza kuwa hii ni njia anayotumia kwa kuchafua wasifu wa serikali iliyopo nchini Rwanda.

Mlango iko wazi kwa Nahimana

Mamlaka ya uhamiaji imetoa taarifa inayokanusha madai hayo, ikisema kwamba Nahimana hakuwa kuzuiliwa kurejea lakini anapaswa kutumia njia halali.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments