Watu watatu walikufa na zaidi ya nyumba 800 zimeharibika kwa mvua kali

Watu watatu walifariki dunia na mamia ya nyumba zimeripotiwa kuharibika nchini kote kutokana na mvua kali iliyonyesha jumamosi iliyopita.

Ripoti iliyotolewa na Wizara inayohusika na masuala ya wakimbizi na maafa nchini Rwanda, MIDMAR, inasema kuwa mvua hii iliharibu nyumba 702 wilayani Kicukiro, nyumba 29 katika Kamonyi.

Habinshuti Philipe, afisa anayehusika na maswala ya maafa katika MIDMAR, amesema kwamba vyumba 10 vya mashule ya sekondari wilayani Nyarugenge na hekta 18 za kilimo ziliharibika mno.
Na yeye aliongeza kuwa waathirika wameanza kupatiwa msaada ya dharura.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments