Mzungu wa Unga El Chapo apelekwa Marekani

Mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya raia wa Mexico, Joaquin “El Chapo” Guzman amepelekwa nchini Marekani, serikali ya Mexico imetangaza Alhamis hii.

Aliwasili jijini New York kwa ndege tokea Cuidad Juarez. El Chapo anakabiliwa na kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kuingiza kiwango kikubwa cha dawa za kulevya nchini humo.

Kiongozi huyo wa cartel ya Sinaloa alikuwa ameomba abakie Mexico lakini ombi lake limekataliwa. Yupo kwenye ulinzi mkali sababu amewahi kutoroka mara mbili kwenye magereza yenye ulinzi mkali nchini Mexico.

Atapandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Brooklyn Ijumaa hii.

El Chapo anaaminika kujipatia mabilioni ya dola kutokana na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments