Uuzaji haramu : Suala la wamasai kutafutiwa suluhu kidiplomasia

Mji wa Kigali umeanza vuguvugu za kuwaondoa wauzaji wanaouzia mtaani ili kuwahimiza kufanya biashara halali.

Kwa hivyo, Mji wa Kigali umeweka sheria inayotaraji adhabu ya Rwf 10,000 kwa muuzaji na mteja wake.

Akiongea na wanahabari jana kwenye ofisi ya mji wa Kigali, Bi. Patricia Muhongerwa, afisa wa ustawi wa jamii, alisema kuwa na ishu ya wamasai wanaouzia mtaani itashughulikiwa suluhu lakini Wao hawatafanyiwa kama wanyarwanda.

Yeye alisema kwamba Rwanda ni nchi iliyokubali free movement of people na hii ndo sababu suala la wamasai litashughulikiwa kidiplomasia pamoja na ubalozi wa taifa wanapotoka ili na wao waheshimu vigezo na masharti ya kufanya biashara nchini Rwanda.

Jiji la Kigali husema kwamba kuondoa wauzaji mtaani ni mpango muhimu unaolenga kuweka usafi kibiashara na kuimarisha usalama na kuhimiza yeyote anayefanya biashara kwenye ardhi ya Rwanda kulipa kodi.

Patricia Muhongerwa, mjibika wa masula ya ustawi wa jamii mjini Kigali

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments