Viongozi wa kidini watakiwa kutumia ushawishi wao kwa kukabiliana na unyanyasaji kijinsia

Wizara ya usawa wa kijinsia na ustawi wa jamii ilitoa wito kwa viongozi wa kidini kutumia ushawishi wao kwa kukomesha unyanyasaji wa kijinsia unaondelea kuongezeka nchini Rwanda.

Katibu kudumu wa wizara hiyo, Bi Nadine Umutoni Gatsinzi alisema kwamaba umuhimu wa viongozi wa kidini wa kukabiliana na tatizo hilo hauwezi kusahaulika.
Yeye alisema hayo katika tukio lililoandaliwa na shirika la vyama vya kutetea haki za kibinadamu nchini Rwanda CLADHO.

Utafiti uliofanywa mwaka wa 2014/15 ulionyesha kuwa kiwanga cha kunyanyasa watoto wakiwa katika miaka ya utotoni kiliongezeka hadi asilimia 7.3 katika mwaka wa 2015 kutoka 6.1 mwaka 2010.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments