Mfalme Kigeli V Ndahindurwa azikwa

Jana ndipo Mfalme wa mwisho wa Rwanda Jean Baptiste Ndahindurwa alipozikwa katika eneo la Mwima karibu na kaburi ya ndugu yake Rudahigwa.
Msafara mkubwa wa waliokuja kutoa heshima za mwisho kwa Kigeli V wamekusanyika katika hospitali ya king Faisal kabla ya kueleka Mwima kusini mwa Rwanda.

Mfalme Kigeli alikuwa akiishi uhamishoni mjini Washington, nchini Marekani tangu mwaka 1992, na aliaga dunia Oktoba 16 akiwa na umri wa miaka 80.

Mfalme wa mwisho wa Rwanda, Kigeli wa 5, aliyetimuliwa madarakani tangu miaka hamisini iliyopita, aliishi uhamishoni nchini Marekani tangu mwaka 1992.

Mfalme Kigeli wa 5 alihamia nchini Marekani tangu mwaka 1992, baada ya kuishi miaka kadhaa nchini Tanzania, Uganda na Kenya.


Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments