Mwili wa mfalme Kigeli wawasili Rwanda

Mwili wa mfalme wa mwisho nchini Rwanda, Kigeli wa 5 umewasili Jumatatu hii mjini Kigali, nchini Rwanda baada ya kesi ya mahakama kati ya familia yake, kuhusu ni wapi angezikwa.

Kifo cha mfalme Kigeli kilizua mzozo ndani ya familia, kati ya ile inayoishi nchini Marekani na iliyo nchini Rwanda kuhusu ni wapi angezikwa kabla ya mahakama ya Marekani kutoa hukumu kuwa atazikwa nyumbani kwao.

Mfalme Kigeli alikuwa akiishi uhamishoni mjini Washington, nchini Marekani tangu mwaka 1992, na aliaga dunia Oktoba 16 akiwa na umri wa miaka 80.
Mfalme wa mwisho wa Rwanda, Kigeli wa 5, aliyetimuliwa madarakani tangu miaka hamisini iliyopita, aliishi uhamishoni nchini Marekani tangu mwaka 1992.

Mfalme Kigeli wa 5 alihamia nchini Marekani tangu mwaka 1992, baada ya kuishi miaka kadhaa nchini Tanzania, Uganda na Kenya.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments