Rwanda inajiandaa kupokea vifaru weusi.

1

Mshauri wa kwanza katika ubalozi wa Rwanda nchini Uholanzi Bw Robert Kayinamura ametangaza kuwa maandalizi ya kuwapokea wanyama hao 2o kutoka mbuga ya wanyama ya Tha Tholo iliyopo mkoani Limpopo nchini Afrika kusini unakaribia kutamatika.

Bw Kayinamura ameliambia gazeti la the newtimes kwamba mpango wa kurudisha wanyama aina vifaru weusi waliokosekana katikia Akagera National Park miaka kibao ya nyuma unatarajiwa kufika mwisho mwezi februari kwa hisani ya serikali ya Uholanzi ambayo ilitoa kiasa cha fedha za Euro 200,0000 mwaka jana.

Yeye aliongeza kuwa hawa wanyama 20 ( 10 wa kiume na 10 wa kike) watasafirishwa nchini Rwanda katika vipengele viwili ambapo kundi moja litakuwa na wanyama 10.

Bodi ya Maendeleo nchini Rwanda inasema kuwa huu ni mojawapo wa mipango inayolenga kuongeza idadi ya watalii.

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments