Rais Paul Kagame anasubiriwa nchini India.

Rais Paul Kagame akipeana mkono na mwenzake wa Uhindi Mhe. Pranab Mukherjee

Rais Paul Kagame anasubiriwa nchini India katika ziara ya kazi itakayoanza mwezi Januari, 09-12 mwaka huu.

Yeye atahudhuria mkutano wa Vibrant Gujarat global Summit utakao kuwa ukifanyika kwa mara ya nane mjini Gandhinagar katika jimbo la Gujarat lililopo magharibi mwa Uhindi ndani ya ukumbi wa Mahatma Mandir.

Rais Paul Kagame ambaye atahudhuria mkutano huo kwa mwaliko wa waziri mkuu Narendra Mondi, anatarajiwa kufanya mazungumzo ya faragha na waziri huyo tarehe 09 kabla ya mkutano kuanza.

Mkutano ambao hujadili masuala ya biashara, utahudhuriwa pia na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta na washiriki wengi kutoka mataifa mbalimbali.

Jengo litakalopokea mkutano

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments