Kayonza watu watano wameshikiliwa juu ya makosa ya ubadhirifu.

Wanachama watano wa ushirika wa kilimo cha mpunga Duterimbere -Murundi, wilayani Kayonza wametiwa nguvuni jumanne iliyopita juu ya makosa ya ubadhirifu.

Hao waliokamatwa wamo Evariste Niyioreba, rais wa Duterimbvere-Murundi na Pauline Mukashimwe, meneja wengine ni Gido Nyandwi, mratibu wa mavuno, Mary Hangayika, mshauri na Jerome Uwihanganye, katibu.

Hii bodi ya uongozi wa Duterimbere-Murundi inashukiwa ubadhirifu wa pesa sawa na Rwf 8.5 milioni.

Msemaji wa jeshi la polisi mkoani wa mashariki mwa Rwanda, Emmanuel Kayigi ameliambia gazeti la The newtimes kwamba washukiwa wamepelekwa kituoni cha polisi kilichopo Rukara.

Duterimbere-Murundi ina wanachama 1,576 na hulima mpunga kwenye hekta 400 za kinamasi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments