Hakimu ameamuru kupeleka mwili wa Kigeli V nchini Rwanda.

Mahakama nchini Marekani katika jimbo la Viriginia imeamuru kupeleka mwili wa mfalme Kigeli V Ndahindurwa nchini Rwanda ambapo anatarajiwa kuzikwa hapo Nyanza, kusini mwa Rwanda.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya siku mbili hakimu akisikia pande mbili zilizo tofautiana kuhusu eneo la kaburi ya Kigeli, pande moja ikitaka mfalme azikwe uhamishoni, nyingine ikitaka yeye azikwe nchini Rwanda.

Hakimu amesema kuwa maiti ya Kigeli inapaswa kupelekwa Rwanda kwani watu waliotaka mazishi ya Kigeli V Ndahindura kufanyika uhamishonin hawana ushahidi tosha wa kufafanua ombi lao.

Mfalme huyo alitawala Rwanda kwa miaka miwili tu kwanzia mwaka 1959 hadi 1961 wakati utawala wa kifalme ulipong’olewa kupitia kura ya maamuzi na kumlazimisha kwenda uhamishoni.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments