Wakili Toy aliyeuawa kwa kupigwa risasi atolewa heshima za mwisho

Jeneza lenye mwili wa Me Toy limekuwa katika mjengo wa mahakamani kuu

Wanasheria kadhaa wamejumuika katika jengo la mahakama kuu kwa kutoa heshima zao za mwisho kwa Wakili Ntabwoba Nzamwita Toy aliyeuawa kwa kupigwa risasi na askari wa polisi usiku wa kuamka Jumamosi iliyopita mbele ya jengo la Kigali Convention Center mjini Kigali baada ya kuhasamiana na polisi akitaka kuingia ndani kwa nguvu.

Me Toy alisomea mashule ya msingi na sekondari katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na chuo kikuu cha Rwanda. Yeye alifariki akiwa na miaka 49 na watoto wanne.

Mjane wa Nzamwita

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments