Ruhango : Viongozi 20 wa ngazi za chini wamejiuzulu

Makuruki.rw imefichuliwa kuwa zaidi ya viongozi 20 wa ngazi za chini wilayani Ruhango, kusini mwa Rwanda wamejiuzulu.

Mwanachama mmoja wa halmashauri wilayani humo ameiambia makuruki.rw kuwa viongozi waliojiuzulu ni kati ya 20 na 27 kwa sababu zisizo fahamika hadi leo.

Mkuu wa halmashauri ya Ruhango, Bw Rutagengwa Jerome amesema kwamba yeye hajui iwapo hao viongozi wametangaza kujiuzulu ingawaje wao wanafaa kujiuzulu kwani wao walishindwa kutumika majukumu yao vyema, yaani kuhamasisha raia kulipa bima ya kijamii.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments