Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Gambia akimbilia mafichoni

Alieu Momar Nji, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Gambia.

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Gambia, Alieu Momar Njai, ameondoka nchini, kwa mujibu wa ripoti kadhaa. Familia yake imefahamisha BBC kuwa hayupo nchini Gambia, na kamwe haitofichua eneo ambapo amekimbilia .

Inaarifiwa kuwa Alieu Momar Njai alikimbilia mafichoni kufuatia vitisho vya kuuawa baada ya kutangazwa kushindwa kwa Yahya Jammeh katika uchaguzi wa urais.

Rais anayemaliza muda wake kwa mara ya kwanza alikubali kushindwa na kupongeza ushindi wa mpinzani wake Adama Barrow, lakini baadae alipinga ushindi huo na kuitaka mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais, akisema uchaguzi uligubikwa na kasoro nyingi.
Tume ya Uchaguzi ilitangaza kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments