Mwanzilishi wa gazeti la Rwanda focus akamatwa

Shyaka Kanuma, mmiliki wa Rwanda focus limited inayomiliki Gazeti la Rwanda focus, akamatwa akidaiwa kukwepa kulipa kodi na udanganyifu katika upewaji wa soko la Rwanda Demobilisation and reintegragtion commission ; polisi imethibitisha.

Lynder Shyaka, naibu msemaji wa Polisi ameliambia gazeti la the newtimes kwamba Shyaka alikamatwa jumamosi iliyopita na anafungwa katika kituo cha polisi kilichopo Remera, mjini Kigali.

Shyaka Kanuma anadaiwa kukwepa kulipa kodi sawa na Rwf 65 milioni na kutolipa zaidi ya Rwf 18 milioni kwa watu mbalimbali na wakiwemo na wafanyakazi wake.

Kanuma alitiwa nguvuni baada ya kufunga mlango ya kampuni yake hivi karibuni.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments